Translations:Campaigns/Foundation Programs Team/56/sw
Appearance
From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
Zawadi au tuzo ni muhimu kwa mashirika ya kujitolea kama vile Wikimedia. Ni njia mojawapo ya kutoa motisha au kuhimiza ushiriki endelevu. Hata hivyo, mara nyingi ni vigumu sana kuamua juu ya nini kinaweza kuwa zawadi bora kwa kampeni. Tumesikia wasiwasi na tumeulizwa maswali kuhusu kwa nini aina fulani za tuzo au zawadi hutolewa kwa baadhi ya kampeni. Jiunge nasi kujadili na kuelekeza mazungumzo kuelekea falsafa iliyo wazi zaidi na thabiti ya zawadi kwa kampeni ndani ya Vuguvugu la Wikimedia.